Ujumbe wa ubalozi wa taifa la Sweden Humu nchini umezuru kaunti ya Pokot Magharibi ili kukagua miradi ya maendeleo chini ya usimamizi wa mashirika ya kibinafsi ili kuhakikisha wakaazi kwenye maeneo kame wanafaidhika kwa miradi hizo na kujiendeleza kimaisha.
Ukiuongwa na balozi Caroline Vizine ujumbe huo unasema mataifa ya Sweden na Kenya unalenga kubadilisha maisha ya wakaazi kwenye maeneo kame na ambazo yamekumbwa na uvamizi na wizi wa mifugo akisema ni kupitia miradi hiyo itawezeshwa kupitia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake gavana wa kaunti hiyon Simon Kachapin amepongeza taifa hilo akisema wenyeji kaunti hiyo watanufaika kutoka na mradi huo chini ya shirika la World Vision.