Kadinali mwadhama Yohane Njue amewataka majandokasisi na makleri kujitwika jukumu la kuhudumu katika shamba la bwana kwa maelekezi ya sheria za kanisa.
Akiongea wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka ishirini na mitano ya utumisha wa watawa wa shirika la Felician dyosisi ya Embu,mwadhama Njue amekaririr haja ya watumishi hao kumakinikia utendakazi wao na kuepukana na maswala ambayo huenda yakawasongesha mbali na mwenyezi mungu.
Amesema kuna changamoto si haba wakati wanaendeleza shughuli zao ila wanapaswa kusimama imara ili waweze kuwaelekeza waumini kwa njia mwafaka wa kuitwa wana wa mungu.
Kadinali Njue amesisitiza umuhimu wa kila mja kumtolea shukrani mwenyezi mungu kila wakati katika shughuli zao za maisha akiashiria kwamba miito mbalimbali walizo jaliwa zote zimetoka kwake mwenyezi mungu.