Heshimuni Familia zenu

Askofu wa jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi ametoa wito kwa Kila mmoja kuheshimu na kupenda familia.

Akihubiri katika Misa ya kusherehekea miaka ishirini na Tano ya utendakazi katika shamba la bwana la padre Fredrick Njoroge askofu Obanyi amesema kuwa Mungu hutumia familia kutekeleza wokovu wake kwa kuwa hiyo familia ndio nguzo muhimu na chombo anachotumia Mungu kutekeleza wajibu wake.

Ametoa wito kwa wazazi kuwaheshimu na kuelekeza Wana wao kwa kuwa watoto hao wanaweza kuelekeza wazazi na hata jamii katika njia ya wokovu.

Amewataka mapadre kutumia wito wao kuwabariki na kuwaonyesha wakristu na wale walipoteza njia ramani ya Imani ili wapate neema zake mwenyezi Mungu.

Askofu kadhalika amewataka wazazi Kila wakati kunena Yale yaliyomema kwa watoto wao siku zote akitoa wito kwa wale walio na majukumu ya kuongoza familia kutetea familia kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *