KCCB yataka amani Sondu

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB limetoa wito kwa asasi za usalama na idara zote husika kumakinikia swala la kuleta amani na uwiano miongoni mwa wakenya.

Katika taarifa iliyotolewa na naibu mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia  Makumba, baraza hilo limetoa wito kwa serikali kufanya upesi na kurejesha amani katika eneo la Sondu mpakani pa kaunti YA Kericho na Kisumu, likisema kuwa taifa la Kenya halipaswi kushuhudia mapigano ya kikabila na maafa kama ilivyoshuhudiwa hivi majuzi, likitoa wito kwa ushirikiano baina yua viongozi wa kisiasa na hata wale wa kidini.

Baraza hilo kadhalika limetaka serikali kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wakenya kulekea uchaguzi mkuu likisema kuwa kupanda kwa gharama ya maisha nchini imesakama wakenya wengi, wengi wao wakishindwa kupata bidhaa za kimsingi kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Kadhalika wametoa wito kwa serikali kushughulikia swala la ukosefu wa ajra miongoni mwa vijana nchini badala ya kutumia visivyo rasilimali, wakishauri serikali kukatisha ziara za nje ya nchi zisizostahili, kama njia moja ya kupunguza utumizi mbaya wa mali ya umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *