Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang amewaonya mawaziri na maafisa wakuu dhidi ya ufisadi na utepetevu kazini ambao umechangia kuchelewa kwa huduma na miradi mbalimbali kaunti hiyo.
Akizungumza mjini Kapsabet baada ya kuongoza hafla ya kutia sahini mkataba ya utendakazi baina ya mawaziri , wakurugenzi pamoja na maafisa wengine wakuu serikalini gavana sang ametoa ilani kwa baraza lake la mawaziri na maafisa wakuu kwamba hatakosa kuwatimua kazini iwapo watalegeza majukumu yao.