Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet ilizindua mpango wa bure ya kuwachanja kondoo na mbuzi katika maeneo ambayo kiwango ya joto hiko juu kama njia moja ya kuwakinga dhiti ya magonjwa.
Akizindua mpango huo katika eneo la Kabulwo eneo bunge la keiyo Kaskazini gavana wa kaunti hiyo Wesely Rotich alisema kuwa mpango huo utatakelezwa katika wadi 6 ambazo ziko kwenye hatari za kukumbwa na mkurupuko wa ugonjwa wa mifugo.
Rotich alidokeza kuwa kupitia mpango huo itawasaidia wakulima kuboresha ufugaji wa mbuzi na kondoo ili waweze kujikimu kimaisha