lalama za wanaoishi na ulemavu

Watu wanaoishi na changamoto za kimwili katika eneo bunge la Marakwet magharibi kaunti ya Elgeyo Marakwet waliandamana  hii leo  wakitaka  matakawa yao yatekelezwe ipasavyo  hasa shuguli ya usajili  likiendelea katika kaunti hiyo .

Watu hao walisema kuwa nafasi ambazo wametengewa ni chache ikilinganishwa na idadi yao,jambo ambalo wametaka serikali kuingilia kati ili wao wapate haki yao.

Haya yanajiri wakati ambapo serikali inaendela kusisitiza haja   wazee  na watu  wanaoishi na ulemavu  kujitokeza kusajiliwa  kwa mpango wa inua jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *