Zaidi ya watu 3000 wamekesha kwenye baridi baada ya moto kuteketeza nyumba zao kwenye eneo la Kibish, Turkana kaskazini, mpakani mwa Kenya na Ethiopia usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chifu wa eneo hilo David Erkudi, hakuna aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo japo mali ya thamani isiyojulikana imeteketea.
Haijabainika kiini cha moto huo huku familia zilizoathirika zikitoa wito wa msaada wa mavazi na chakula. Huu ni mkasa wa pili kutokea eneo hilo katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya mkasa sawia kutokea mwaka jana japo familia chache tu zilizoathirika.