Askofu mkuu wa Kiangikana nchini Jackson Ole Sapit amewataka viongozi wa kisiasa hasa Rais William Ruto na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kuweka kando tofauti zao na kutatua maswala yanayohusu taifa kwa njia ya amani.
Ole Sapit ameweka wazi kwamba taifa hili ni muhimu zaidi kuliko wawili hao na malumbano ya kila mara kwenye majukwaa mbalimbali baina ya wawili hao na viongozi wengine inasikitisha mno na sharti suluhu la maridhiano kuafikiwa.
Askofu Sapit alisikitikia namna viongozi ambao wakenya waliwaenzi kukosa kuwasikiza katika uwepo wa uwiano kwa hili akisema sharti mazungumzo na amani ipatikane.
Kadahalika,Ole Sapit alisema kwamba kama viongozi wa dini waikuwa wamehisi kwamba maelewano ungepatikana ila hatua ambayo viongozi wa kisiasa walikuwa wamechukua na kuwashauri kuzingatia kukaa chini na kutatua mzozo baina yao kwa manufaa ya mkenya wa kawaida na ukuwaji wa uchumi wa taifa hili.