Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Eddyson Nyale amewaomba wazazi ambao wanahusishwa na sakata ya masomo kule Ufini na Canada kuipa idara ya usalama muda kujadiliana na washikadau waliohusika na mpango huo kabla ya wao kuchukua hatua kali za kibinafsi.
Akiongea na wazazi ambao ni waathiriwa wa mpango huo nje ya afisi yake mjini Eldoret aliwahakikishia wazazi hao kwamba anamini suluhu la kudumu litapatikana na kila mmoja aweze kupata haki.
Ameweka wazi kwamba amezingatia kuipa muda wake kubwa kufanya maongezi na viongozi mbalimbali kaunti ya Uasin Gishu mwishoni mwa juma hili na kuafikiana kwao kwa njia zinazostahili kufuatwa.
Hapo awali wazazi pamoja na wanao wenye ghadabu walifika kwenye afisi za kamishna wakimtaka kuwasaidia kutatua swala hilo.
Yanajiri haya baada ya serikali ya kaunti ya Uasin Gishu hapo awali ikiongozwa na aliyekuwa gavana Jackson Mandago na gavana wa sasa kudaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa za wazazi ambao walikua kwenye maelewano na serikali kwa wanao kueelekea katika mataifa za nje kwa masomo hususana mataifa za Ufini na Canada na hadi wa sasa wapo wale ambao wanaosema wanao hawakuwai soma kwenye mataifa husika ila walikua wameshinda wakiangaikia kupata kibali katika mataifa hayo.