Tabua afya yako

Wakaazi wa kaunti ya Nandi wameshauriwa kufika mapema katika vituo vya afya ili kufanyiwa ukaguzi wa  kiafya kama njia moja ya kubaini magonjwa sugu haswa ule wa saratani.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa barabara na uchukuzi kaunti hiyo Drice Rono ambaye alisema kuwa tayari serikali ya kaunti ya Nandi imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa matibabu ya ugonjwa wa saratani utafanywa katika kaunti hiyo, akitoa wito kwa kila mkaazi wa kaunti hiyo kuwa na mazoea ya kufanyiwa ukaguzi.

Ikumbukwe kuwa shirika la misaada mapema mwaka huu lilibaini kuwa Wanawake walio na umri wa miaka 30 walio na historia katika familia ya jamaa zao kuugua saratani ya matiti, wanapaswa kufanyiwa ukaguzi wa kila mwaka kubaini mapema iwapo wanaugua ugonjwa huo au la

Shirika hilo kwa jina Breast Cancer Now limefadhili utafiti uliobaini kwamba saratani hutambulika mapema wakati wanawake wenye umri wa kati ya miaka 35 hadi 39 walio katika hatari ya kuugua wanapofanyiwa ukaguzi wa kila mwaka yaani mammograms.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *