za mwizi arobaini

Polisi hapa mjini Eldoret wamemkamata mshukiwa wa nne anayehusishwa na mauaji ya kinyama dhidi  ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 20 jijini Nairobi.

Benjamin Njenga ambaye ni mhudumu wa matatu mjini Eldoret alitorekea kujificha jijini Nairobi baada ya kudaiwa kushirikiana na wenzake watatu kwa kumuua Mohamed Ismael.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kwamba mshukiwa alishiriki kitendo hicho cha kinyama kwa ushirikiano na wenzake  watatu mwezi Juni tisa katika mtaa wa West indies kaunti ndogo ya Turbo kaunti ya Uasin Gishu.

Njenga amefikishwa mahakamani na hakujibu shtaka lolote baada ya upande wa mashtaka kuomba azuiliwe kwa siku saba zaidi katika kituo cha polisi cha Central huku wakiendelea na uchunguzi.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kwamba washukiwa hao wanne walimgonga kwa mawe marehemu akiwa nje ya lango kuu la bweni lao huko West Indies.

Mshukiwa huyo sasa atafikishwa mahakamani tarehe 15  mwezi ujao wa Agosti ambapo atasomewa mashtaka.

Wakati huo,washukiwa wengine watatu wanahusishwa na mauaji hayo watatu akiwemo Juliet Ayieta ,Paul Osinde na Gregory Mukhori ambao wamekuwa wakizuiliwa kwenye gereza la Eldoret GK baada ya kufikishwa mbele ya jaji Reuben Nyakundi,huku upande wa mashtaka ukiambia mahakama kuwa watatu hao baada ya kufanyiwa uchunguzi wa akili katika hospitali wa rufaa ya Moi Eldoret na wako tayari kusomewa mashtaka yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *