Himizo limetolewa kwa wakristu kukuza imani yao kwa kujitolea na kujitenga na maswala ambayo yanaweza kuwaweka mbali na mwenyezi mungu.
Akizungumza wakati wa hafla ya daraja ya upadrisho katika eneo la Karen jijini Nairobi,mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Kenya na Sudan Kusini Mwadhama Hurbatus Maria Van Megen, amesisitiza haja ya wao kuelewa kikamilifu kwamba kila wakati mwenyezi mungu anawapa muda wa kuipalilia imani yao na hivyo kuwa tayari kumpokea huyo kristu.
Alisema kwamba kila kiumbe katika ulimwengu huu anajukumu lake kwa njia iliyo tofauti, na hivyo wakiungana mikono wataweza kujikwamua kwenye mauti na kusonga mbele kiimani.
Vilevile,mwadhama Van Megen aliwaomba wakristu kutilia maanani kuwa waaminifu kwa sala ndipo wasimame imara katika imani hiyo.