SIGNIS;Waandishi katoliki wawe na huruma zaidi kwa wahamiaji

Warsha la SIGNIS  Afrika kuhusu wahamiaji na wakimbizi limemalizika mjini Kampala, Uganda kwa kutayarisha rasimu ya kile ambacho hatimaye kinapaswa kutambulika kama miongozo ya kitaalamu ya kutumiwa na vyombo vya habari vya Kikatoliki barani Afrika wakati wa kuripoti kuhusu wahamiaji na wakimbizi. Hata hivyo Kamati itaundwa kwa kazi zaidi ya rasimu hiyo.

Katika siku ya mwisho ya sehemu ya warsha hiyo iliyaonza tarehe 11 Julai 2023, wahusika wa vyombo vya habari kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda walishirikiana na washiriki katika majadiliano juu ya nini kifanyike ili kuhimiza ripoti za kitaalamu na za huruma ambazo bado ni za kweli na zenye lengo kuu. Swali la ni nini kinachomtofautisha mwanahabari Mkatoliki wa Kiafrika lilijadiliwa kwa kwa kirefu zaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *