KANISA LATAKA AMANI

Viongozi wa kidini wametoa wito kwa rais William Ruto na kinara wa muungano wa upinzani Raila Odinga kushiriki mazungumzo ili kukwamua mgogoro unaoghubika taifa.

Katika kikao na wanahabari viongozi hao wa kidini wamemtaka rais William Ruto kusikikza sauti ya wakenya kwa kutathmini upya mswada tata wa kifedha wa mwaka wa 2023, wakisema kuwa hali ya juu ya kiuchumi inayoshuhudiwa kwa sasa huenda ikawasakama wakenya hii hapa na mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa katoliki nchini askofu Martin Kivuva Musonde.

Viongozi hao kadhalika wametoa wito kwa kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Raila Odinga kusitisha misururu ya maandamano ambayo yameratibiwa kufanyika juma lijalo wakisema kuwa maandamano hayo yataitumbukiza taifa katika machafuko. Wametoa wito kwa wakenya kutokubali kuchochewa na wanasiasa na badala yake washirikia katika mdahalo utakaofanikisha mshikamano wa taifa hii hapa ni kiongozi wa SUPKEM Hassan Ole Nado.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *