Afya nzuri uinjilishaji bora

Askofu wa jimbo katoliki la kitale Henry Juma Odonya amewataka wahudumu wa afya kutumia fursa waliyopewa ya kuwahudumia wagonjwa kwa upole na unyenyekevu.

Akiongea katika parokia ya Mtakatifu Patrik Kibomet wakati wa ufunguzi wa zahanati ya watawa wa Nazareth cha St.Paul Kipkorion,askofu Juma alisema ni fursa ya kipekee ambayo wahudumu wa afya walipewa kuwasaidia binadamu ikizingatiwa kwamba miili za wanadamu zimesheheni magonjwa na usaidizi wao utachangia pakubwa katika uenezaji wa injili wake kristu.

Aliwashauri wahudumu hao kutoa huduma zao basi na ubaguzi wowote kwani anasema wanayo uwezo wa kuwapa fursa nyingine ya maisha kwa wale  wagonjwa walio hali mahututi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *