Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imehimizwa kuhakikisha kwamba vyam vya ushirika vina nawiri katika utendakazi wake na kuwafaidi wanachama kwa miaka mingi zijazo.
Kulingana na katibu katika wizara ya michezo Peter Tum akiongea wakati wa hafla ya siku ya ushirika mjini Eldoret,vyama vya ushirika ni vya manufaa kubwa kwa wananchi na hivyo sharti serikali za kaunti kuzilinda kwa kuwepo kwa sera zitakazozipa mwongozo bora ndipo ziweze kusimama imara.
Alimtaka gavana wa kaunti ya Uasin Gishu kushirikiana na washikadau kutoka sekta ya biashara ndipo waweze kulinda vyama hivyo na kupata mwelekeo ulibora na kusaidia vyama na wanachama wake kutimiza malengo yao ya maisha na kibiashara.
Alieleza kwamba vyama vya ushirika ni vya manufaa mno na wafanyibiashara wamepata fursa nzuri kujisimamia na kujijenga maishani mwao kupitia vyama hivyo na kupanua biashara zao.