Amani itarejea Kerio

Muungano wa maaskofu wa kanisa katoliki kutoka katika eneo pana la kaskazini mwa bonde la ufa ambayo yamekuwa yakishuhudia vurugu umeapa kushirikiana ili kutafuta amani katika maeneo hayo.

Katika taarifa iliyosomwa kwa niaba ya maaskofu hao na askofu wa jimbo katoliki la Lodwar askofu John Mbinda muungano huo sasa umeapa kushirikisha  jamii moja kwa moja pamoja na wale waliokengeuka kutoka katika visa hivyo vya uhalifu na kuandaa mikutano ya kila mara ili jamii iweze kuhamasishwa dhidi ya machafuko.

Maaskofu hao kadhalika waliapa kuweka mikakati itakayo washirikisha wadau wote pamoja kama njia moja ya kutwaa silaha haramu zilizo mikononi mwa raia, na hata kuandaa mikutano ambayo yatalenga kuleta maridhiano miongoni mwa jamii, hii hapa ni askofu wa jimbo la kitale askofu Juma Odonya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *