Wito umetolewa kwa kitengo cha kanisa katoliki cha kuwajali wasiojiweza katika jamii Caritas kuonyesha upendo kwa wale ambao mara nyingi wametengwa katika jamii.
Akizungumza katika Jumba la Kardinal Otunga wakati wa mkutano wa kila mwaka wa Caritas askofu mkuu wa jimbo kuu la Niarobi Philip Subira Anyolo amesema kwamba wapo watu wengi ambao wametelekezwa katika jamii swala analosema yawapasa kama kikundi kuwakaribia na kuwapa usaidizi kwa uwezo wao.
Vilevile,askofu mkuu amebainisha kwamba wasiojiweza na waliotengwa katika jamii wanapaswa kuonyeshwa upendo ndipo nao wahisi ujamaa na kuweza kuendelea na maisha yao kama wakenya wengine.
Aisha,askofu Anyolo amewataka kuwa mstari wa mbele kulieneza neno lake mwenyezi mungu kwa kila mmoja bila ya ubaguzi wowote.
