Uasin Gishu Wakosoa Ruto

Hisia mseto zimegubika baada ya rais William Ruto kutia Saini mswada wa fedha mwaka wa 2023 huku baadhi ya wakaazi hao wakiunga mkono wengine wakitofautiana nao.

Wakizungumza mjini Eldoret ,baadhi ya wenyeji hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Oscar Shikanga ni kwamba kufuatia hatua ambao rais alichukua inaashiria kwamba wakenya wawe tayari kupambana na hali ngumu ya maisha hata zaidi kwani ameeleza kwamba bei ya bidhaa muhimu itapanda kutokana na kuongezwa kwa ushuru kwa mafuta ya petrol.

Wakaazi hao vilevile wamesema kwamba itakua jambo la busara iwapo rais Ruto atazingatia kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni ya kuwakwamua wakenya kutoka kwa lindi la umaskini ndipo mkenya mlalahoi aweze kujiinua kupitia biashara yake ama hata ukulima.

Wananchi hao pia hasa wale wanaounga mkono hatua hiyo wanasema kwamba ni hatua ya muhimu sana kwani itasaidia taifa kujisimamia na wakenya waweze kujisimamia kwa miaka zijazo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo serikali imeweka mpangoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *