hamasisho kuepuka pombe haramu

Ipo haja ya kila mwanajamii kupata kuhamasika kikamilifu na kujitenga na ubugiaji na unywaji wa pombe.

Ni kauli yake askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ambaye anasema kwamba jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wale ambao hawajapata fursa ya kuelekezwa ipasavyo dhidi ya unywaji wa pombe kwani anasema familia nyingi zimesambaraitka kutokana na hulka hii.

Akiongea katika eneo la Chogoo katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet wakati wa mazishi ya Mwalimu Paul Chelimo ,askofu aliwatahadharisha sana wanajamii dhidi ya kuwapuuza wale amabao wameonekana kuzama katika uraibu huo ambao anasema vijana wengi wamezama mno na hata kujipata hawana jambo la manufaa kufanya katika maisha yao.

Alisema kwamba familia nyingi zimesambaratika kutokana na tabia hii akisema yawastahili sio tu wanafamilia ila kwa jamii kwa ujumla kuwasaidia watu hao kubadili mienendo hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *