Toeni leseni kupitia wenyeji

Wenyeji katika eneo la Block 4 mtaani Langas katika viunga vya Eldoret wanaitaka idara ya usalama katika kaunti ya Uasin Gishu kuhakikisha kwamba usalama eneo hilo inaimarishwa kwani wanasema utovu wa usalama umekithiri sana.

Wakiongozwa na kiongozi wa Nyumba kumi Rose Wambui na mzee wa mtaa eneo hilo John Mwaura wamelalamikia mno utovu wa usalama kwani wanasema mataa za barabarani hazipo huku ikiwalazimisha wenyeji hao kufunga biashara zao mapema na kusalia manyumbani kabla ya giza kuingia la sivyo watakabiliana na wahalifu ambao mara si moja huwapora na kuwaumiza.

Wenyeji hao vilevile walimtaka kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu kuhakikisha wamemhamisha maafisa wasimamizi wa kituo cha polisi cha Langas kwa kile wanasema wamezembea kazini.

Walitaka hatua za haraka kuchukuliwa dhidi ya wafanyibiashara wa pombe haramu ambao anasema wamechangia pakubwa utovu wa usalama.

Wakati huo,wenyeji hao walishinikiza kwamba idara inayosimamia utoaji leseni katika kaunti kuhakikisha wanaanda kikao na wenyeji kabla ya kutoa cheti cha kuwaruhusu wafanyibiashara wa pombe leseni kwani wanasema wanaufahamu kamili wa wale ambao wanastahili kuendelea biashara hiyo bila ya kuwatia hatarini wenyeji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *