Mtaala mpya wa Elimu yaCBC unaendelea kusifiwa kwa kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na ufahamu wa mambo msingi katika maisha licha ya changamoto ibuka.
Kulingana na mwalimu wa sekondari ya msingi katika shule ya msingi ya PCEA Kapsoya kaunti ya Uasin Gishu Alfred Rotich, mfumo huo unawapa wanafunzi ujuzi unaostahili wakiwa shuleni na hata nyumbani kuhusu namna ya kukabili hali tofauti za maisha.
Kauli yake imesisitizwa na mwalimu mwenzake Bwire Pauline, anayesema mfumo wa CBC ni rahisi kwa walimu kufunza kwani unahusisha maswala yaliyo bayana kwa wanafunzi.
Hata hivyo, walimu hao wanaisihi serikali kupitia wizara ya elimu kushughulikia changamoto ya uhaba wa walimu, madarasa na vitabu vya kusoma kwa wanafunzi ili kuhakikisha kuwa mfumo huo unafaulu.