Muungano wa maendeleo katika ukanda wa North Rift NOREB Umeweka wazi kwamba unanuia kusaidia serikali ya kitaifa katika kutatua utata wa utovu wa unaoshuhudiwa katika eneo Kerio Valley kupitia ushirikiano wao na washikadau mbalimbali.
Wakizungumza mjini Eldoret wakati wa kutia saini mkataba wa kibiashara cha ukanda huo ,muungano huo unasema kwamba serikali ya kitaifa imefanya juhudi zake ila kwa sasa kama viongozi wa ukanda huo athirika wanapendekeza waweze kufanya mazungumzo ndipo suluhu la muda mrefu uweze kupatikana.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa NOREB ambaye pia ni gavana wa Nandi Stephen Sang,viongozi hao walisema kwamba wataanda mkutano mwezi ujao katika kuweka sera za kudumu kutatua utata huo na kubaini maswala mengine tata yanayojitokeza na yanayoibua tofauti na mtafaruku miongoni mwa wenyeji maeneo yao.
Kadhalika,viongozi hao waliomba ushirikiano uliobora baina ya wenyeji na viongozi wa vitengo vyote ndipo amani ,maendeleo na ujenzi wa taifa kuafikiwa.