ASKOFU OLE SAPI:Tuko tayari kuelekezana kiimani

Askofu mkuu wa kanisa la kiangilikana nchini Jackson Ole Sapit aliweka wazi kwamba viongozi wa makanisa na madhehebu mbalimbali wako tayari kushirikiana na jopokazi lililobuniwa kufuatilia kwa karibu maswala yanayoendeshwa na makanisa kudhibiti wahubiri wa imani potovu.

Akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari Ole Sapit alisema kwamba yapasa jopo liliobuniwa kuhakikisha imeshirikiana kikamilifu na viongozi wote wa kidini ndipo kusishuhudiwe mshikemshike baina yao katika utendakazi wao na kusaidia katika kulineza neno lake mwenyezi mungu.

wakati huo amesema kwamba hawataunga mkono mikakati yoyote ambayo itakwenda kinyume na mafundisho ya kikristu akisema maswala yote ambayo itakikuka imani yen mwelekeo hawataunga mkono kwa vyovyote vile kwani alisema kama viongozi wenye mwelekeo wamekua wakiwaelekeza vyema waumini na ni tu kwa jopo hilo kuhakikisha imewakabili wahubiri wale ambao wanakwenda kinyume na mafundisho matakatifu.

Kadhalika,Ole sapit aliwataka wakenya wote kuungana katika kukabili jinamizi linalojitokeza kuwakumba wanadamu ambayo ni mahubiri potovu na kuweza kumtumikia mwenyezi mungu kila wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *