Wakaazi wa kaunti hii ya Uasin Gishu walitakiwa kukumbatia zoezi la kupanda miti ili kuboresha mazingira na kuepuka na athari zinazotokana na tabia nchi.
Akizungumza Eldoret alipoongoza zoezi la kupanda miti spika wa Bunge la kaunti ya Uasin Gishu Philip Muigei aliwataka wakaazi kuzingira maeneo ambayo miti hiyo hupandwa ili kuzuia kuharibiwa kwa miti hiyo na mifugo, akisema kuwa serikali ya kaunti itatoa vifaa vya kuzingira maeneo yalikopandwa miti katika shule mbalimbali na hata kanisa.
Kadhalika alitoa wito kwa taasisi mbalimbali zikiwemo zile za elimu na hata makanisa kumakinikia swala la upanzi wa miti kama njia mwafaka wa kuboresha mazingira na kadhalika kuafikia malengo ambayo yaliwekwa na rais Willian ruto ya kuepukana na athari za tabianchi.