Wito umetolewa kwa wazazi kuchukua muda wao mwingi kuwapa mawaidha wanao ili wasije wakajuta siku za usoni kwa utovu wa nidhamu kutoka kwao.
Akiongea katika shule ya Queen Of Angels mjini Eldoret,waziri wa teknolojia na maswala ya vijana katika kaunti ya Uasin Gishu Lucy Ng’endo Njoroge alisema kwamba yapasa wazazi kutotelekeza majukumu yao maana wanawajengea wanao maisha bora hapo baadae na kuwa karibu na wanao ni dhihirisho tosha kwamba wanawajali.
Alisema kwamba wanapaswa kutowaachilia wanao kuongozwa na mitandao ya kijamii kwa hili akisema inawapotosha hata zaidi na kuwaomba waweze kufuatilia kwa karibu kile wanafuatilia kwenye mitandao hizo kuwaweka salama dhidi ya kujifunza tabia isiyostahili.
Waziri kadhalika,aliwashauri wazazi kuhakikisha wanatekeleza jukumu lao la malezi na kutowalimbikizia kila jambo walimu akisema kwamba kila mmoja iwe mwalimu au mzazi ana wajibu wake kitofauti.