WEKENI MAZINGIRA BORA YA MASOMO

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT tawi la Tawi la Chepkoilel Sammy Bor ametoa wito kwa wasimamizi wa shule pamoja na walimu wakuu kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira bora kama inavyotatikana na wizara ya afya.

Akizungumza mjini Eldoret, Bor alirejelea visa vya hivi majuzi vya ugonjwa wa kipindupindu katika shule mbalimbali nchini na haswa kisa cha hivi majuzi ambapo wanafunzi wawili na mwalimu mmoja aliaga dunia katika shule ya wasichana ya Mukumu iliyopelekea shule hiyo kufungwa, akitoa wito wa kuwepo kwa usafi wa hali ya juu katika shule hizo kama njia moja ya kuzuia majanga mengi katika shule za humu nchini.

Alitoa wito kadhalika kwa wakuu wa shule kuwa makini na vyakula wanavyonunua kwa wakulima kwa kile anasema kuwa vyakula hivyo mara nyingi vikinunuliwa kabla havijakauka huifadhi sumu kuvu ambayo huathiri wanafunzi.

Katibu huyo ametoa wito kwa wizara ya afya kufanya ukaguzi wa kina katika shule mbalimbali nchini ili kushinikiza shule zote kuwa na mazingira safi kwa wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *