wazee wana usemi mkuu

Swala tata la utovu wa usalama katika bonde la Kerio ukiwa unashuhudiwa na kuzua tumbo joto miongoni mwa wakenya na wakaazi eneo hilo,viongozi wa dini katika kaunti ya Uasin Gishu wakisema kanisa imejitolea kutafuta suluhu ila chanzo kuu ingali haijapatikana huku wakieleza sharti wazee wahusishwe ndipo wafahamu kinachoendelea.

Kwa mujibu wa padre mkuu katika dyosisi ya Eldoret William Kosgey ni kwamba wazee wana usemi mkuu katika jamii na huenda wakifikiwa watasaidia serikali na maafisa wa usalama katika upatikanaji wa amani maeneo hayo.

Kadhalika,alisema kanisa itaendelea kushirikiana na viongozi wengine katika jamii kuafikiwa kwa amani eneo hilo huku akiwaomba wenyeji kuwa na uwazi ndipo amani hiyo iweze kupatikana na waweze kurejelea shughuli zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *