Wizara ya kilimo katika kaunti ya Uasin Gishu kupitia idara ya mifugo na ufugaji wa samaki imeweka mikakati ya kutosha ya kukabiliana na magonjwa yanayojitokeza na kuathiri ukulima wa mifugo yamekabiliwa.
Akiongea mjini Eldoret,katibu katika wizara hiyo Nickson Cheplong amesema sera zipo za kutosha na maafisa kadhaa waliohitimu katika Nyanja ya ukulima wanatumiwa kuwaelimisha wakulima kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo.
Cheplong amesema kwamba kwa sasa wamebaini baadhi ya maeneo ambayo ugonjwa wa miguu na midomo unaibuka san asana na wametoa chanjo kwa mifugo maeneo hayo ili kuokoa mifugo hao wasiangamie.
Wakati huo,katibu huyo alisema kwamba wanapanga kutoa mafunzo kwa maafisa wengi wa kilimo kusaidia katika kupambana na magonjwa ya mifugo na kuhakikisha kilimo cha mifugo inadumu miaka zaidi na kuwasaidia wakulima kujikimu kimaisha.