teknolojia ndio sera ya kudumu

Naibu Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu John Barorot  amewataka wanawake kukumbatia teknolojia kama njia moja ya kujiendeleza.

Akizungumza kwenye hafla ya siku ya wanawake iliyoandaliwa kwenye afisi za kaunti mjini Eldoret ,naibu huyo  alisema kuwa uwezeshaji wa wanawake umepewa kipaumbele katika bajeti ya kaunti ya mwaka huu na kuwahimiza wanawake kuwa waangalifu katika ushirikishwaji wa umma ili kuhakikisha matakwa yao yanazingatiwa.

Hii inaambatana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambao Ubunifu na teknolojia ya usawa wa kijinsia.

Waziri wa wizara ya jinsia na ulinzi wa jamii wa kaunti ya Uasin Gishu Janet Kosgei alisema kuwa ingawa wanawake wamepiga hatua kubwa kwa miaka mingi juhudi Zaidi zinahitajika kufanywa ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unaafikiwa katika nyanja zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *