wito umetolewa kwa madaktari na wahudumu wa afya kuwa makini wanapotekeleza jukumu la o la kuwahudumia wagonjwa.
Ulimwengu ukiadhimisha siku ya wagonjwa dunia mwadhama kadinali Yohane Njue aliwahimiza wahudumu wa afya pamoja na madaktari kuwa makini zaidi wanapotekeleza jukumu lao ili kuhakikisha kuwa kila mgonjwa anasalia salama kwa kuwa wahudumu wa afya wengi wamekuwa wakihusishwa na visa vya utepetevu analosema linapelekea wagonjwa wengi kukosa kuwa na imani na madaktari.
Kadinali Njue kadhalika aliwataka wakristu wote walio na mapenzi mema siku zote kuwaombea wale wanaougua na hata kuwatembelea kuwapa matumaini, kwa kuwa wengi wa wagonjwa wanougua maradhi mbalimbali wameshikwa na unyanyapaa baada ya kutengwa na hata kudhihakiwa na wale walio karibu nao.
Hata hivyo alitoa wito kwa kila mkenya kuwaombea wahudumu hao wa afya ili mwenyezi Mungu awaongoze na kuwatia moyo kila wanapotekeleza majukumu yao kwa kuwa ni vipaji kutoka kwa Mungu.