MISA YA KWANZA YA ASKOFU ODONYA

Askofu mpya wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma Odonya ameadhimisha misa ya kwanza jimboni humo siku moja tu baada ya kusimikwa kwa askofu wa pili wa jimbo hilo.

Askofu Juma ameongoza misa yake ya kwanza jimboni humo katika kathedrali yam aria imakulata jimbo katoliki la kitale ambapo katika homilia yake amehaidi kujisadaka bila kujibakisha ili kuona kuwa waumini wa jimbo hilo wanazidi kuwa kiimani.

Amewataka wakristu wa jimbo hilo kushirikiana naye kwa sala kama njia moja ya kuwavutia watu katika kristu , akimshukuru mwenyezi Mungu kwa daraja hilo la uaskofu.

Askofu huyo mpya kadhalika ametoa wito kwa kila mwanajimbo kujitolea na kumtumikia mwenyezi Mungu katika miito mbalimbali akisema kuwa ni kupitia miito hiyo ndipo kila mja hujenga kanisa kiimani kwa kumtegemea kristu.

Ikumbukwe kwamba askofu Henry Juma anajaza nafasi ya kuwa askofu wa pili wa jimbo la Kitale baada ya kustaafu kwa askofu mwanzilishi wa jimbo hilo Maurice Anthony Crowley.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *