APOSTOLIC NUNCIO :Elimu ni nguzo kwa taifa bora

Wito umetolewa kwa serikali ya kitaifa kuekeza zaidi katika sekta ya elimu ili kuwapunguzia wazazi mzigo mkubwa wa gharamia masomo ya wanao.

Mwakilishi wa Baba Mtakatifu nchini Kenya na Sudan Kusini askofu mkuu  Hubertus Matheus Maria van Megen, alielezea haja ya serikali kukuza ushirikiano wa karibu na kanisa katika kuimarisha elimu nchini.

Akizungumza alipoongoza sheherehe ya kumtawaza na kumsimika askofu mpya wa jimbo Katoliki la Kitale Henry Juma Odonya, askofu mkuu Megen amedokeza kuwa vijana ndio nguzo kuu katika uongozi wa taifa katika siku za usoni na hivyo basi ipo haja ya kuekeza rasilimali za kutosha kuwajengea msingi bora wa elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *