Buni mbinu na sera za kudumu kukabili utovu wa usalama

Padre mkuu wa jimbo katoliki la Eldoret William Kosgei ameitaka serikali ya kitaifa kuweka sera za kutosha kuhakikisha wenyeji katika bonde la Kerio wameishi kwa amani na kurejelewe shughuli za kawaida.

Akiongea afisini mwake mjini Eldoret Kosgei alisema serikali ya kitaifa inaweza ikaweka mikakati ya kuwashughulisha wenyeji hao kwenye miradi ya kimaendeleo kwa kile amesema huenda utovu huo wa usalama unatokana na kukosa kutekelezewa maendeleo kwani ameeleza kwamba juhudi zote za kuwapa amani wenyeji zimewekwa ila bado hali si hali huko.

Alidokeza kwamba japo jukumu la usalama ni la kila mmoja,yapasa serikali kutafuta mbinu nyingine ya kutatua utata huo ndipo wenyeji waweze kuishi kwa amani na warejelee juhudi za kukwamua nchi kwenye lindi la umaskini kupitia kufanya kazi na ukulima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *