serikali yafaa kutafuta mbinu za kukabili utovu wa usalama katika bonde la Kerio

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Centre For Human Rights and Democracy katika kaunti ya Uasin Gishu Kipkorir Ngetich ameitaka serikali ya kitaifa kutumia mbinu tofauti kukabili utovu wa usalama katika bonde la Kerio.

Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,Ngetich alisema kwamba yabainika kwamba utovu huo unazidi kuwa kidonda ndugu hata baada yay a juhudi za serikali kutuliza utovu huo kwa hivyo akaiomba kuhakikisha imeketi chini na washikadau mbalimbali kutoka sekta ya usalama kubuni mbinu hizo zitakazosaidia taifa kukabiliana na wahalifu na wezi wa mifugo.

Alisema kwamba wakaazi wengi wamepoteza maisha yao kutokana na rabsha na vurumai hizo swala analosema limerejesha nyuma juhudi za maendeleo na hata wenyeji kuishi kwa kuhofia maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *