Viongozi wa kisiasa wamehimizwa kuwa mstari wa mbele kuwaunganisha wenyeji kupitia uongozi wao hasa miradi ya kimandeleo na wasije wakawa mabalozi wa ukabila na chuki miongoni mwa wananchi.
Akiongea katika eneo la St.Mathias Matungu County Polythenic kwenye makumbusho ya miaka 25 ya mama Alexandria Khalatanyi ambaye alikuwa mmoja wa watu walioheshimiwa askofu wa dyosisi ya Kakamega Joseph Obanyi amesema kwamba maswala ya maendeleo ni kwa watu wote na sio kwa wale waliowachagua kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa Agosti Tisa mwaka huu bali kwa wote kwa anachosema wakenya wako na uhuru wa kuwachagua wale ambao wanawawenzi.
Aliwaomba viongozi hao kuwa mfano mwema kwa wenyeji na kudumisha ujirani mwema ndipo nao waweze kuwa na heshima ambayo itaweza dumu hata baada ya hatamu ya uongozi wao kukamilika.
Wakati huo,askofu Obanyi amesisitiza haja ya wanafamilia kudumisha na kuhakikisha familia zao zadumu kupitia kwa sala kila muda ambayo amesema itawapa mwongozo uliobora maishani.
Kadhalika,askofu huyo alisisitiza wakristu kuwa na mazoea ya kuwa na moyo wa huruma kwa wengine akieleza hilo litawaongoza vyema kwenye njia ya kuuridhi ufalme wa mbingu.
