KMPDU:Huenda tukafutilia mbali mgomo iwapo kutakuwa na makubaliano

Serikali ya kitaifa imeanzisha mchakato wa kukwamua mgomo wa madaktari ambao umepangwa kuanza mwezi wa Januari mwakani.

Serikali kupitia muungano wa magavana imeandaa mkutano na uongozi wa muungano KMPDU ili kutatua mzozo unaozingira kutotekelezwa kwa makubaliano almaarufu CBA kati ya muungano huo wa madaktari na serikali.

Muungano wa magavana ukiongozwa mwenyekiti wa idara ya afya Muthomi Njuki na mwenzake wa leba Johnson Sakaja umekutana na ULE WA kmpdu ukiongozwa na katibu mkuu Davji Atellah, pamoja na mwenyekiti Abi Mwachi ili kutanzua mgogoro unahusu CBA ambayo kulingana nao wanasema kuwa hadi kwa sasa serikali haijatimiza CBA ya mwaka 2017-2021

Akizungumza na wanahabari katibu mkuu wa KMDU Dr. dAVJI Atellah alisema kuwa wana matumaini kuwa mkutano huu utazaa matunda ambayo huenda ikapelekea KMPDU kufutilia mbali mgomo ambao uliratibiwa kuanza januari mwakani.

Alisema kuwa wameafikia baadhi ya maswala muhimu yakiwemo madaktari kupandishwa vyeo, maswala yanayohusu bima ya afya kwa madaktari na hata nyongeza ya mishahara kwa wahudumu wote wa afya miongoni mwa mengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *