maenedeleo mashinani

Mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet Carolyne Ng’elechei ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuweka fedha katika hazina ya usawi ya maeneobunge, ili kuwasaidia kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwakilishi huyo alikariri kuwa kuna maeneo mengi katika kaunti hiyo ambayo kwa sasa yanakumbwa na baa la njaa, haswa katika maeneo ya Keiyo kusini iliyoko mpakani pa kaunti ya Elgeiyo marakwet na kaunti ya Baringo, akisema kuwa hazina hiyo itapiga jeki juhudi za kutekeleza baadhi ya miradi itakayowasaidia wakaazi hao.

Ng’elechei kadhalika alitoa wito wa ushirikiano kati ya viongozi wote waliochaguliwa katika kaunti hiyo, ili watatue baadhi ya changamoto ambazo zinakumba kaunti hiyo, ikiwemo wizi wa mifugo ambayo hupelekea hata maafa miongoni mwa wale wanaoishi katika maeneo husika.

Aliwataka wale wanaoendeleza utamaduni ya ukeketaji kukoma kufanya hivyo, akisema kuwa tamaduni hiyo inarudisha mtoto msichana nyuma kimawazo, kimasomo na hata kumdunisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *