ASKOFU KIMENGICH:Lindeni watoto dhidi ya dhulma

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich aliwaonya wale wanoavya mimba pamoja na wale wanaowadhulumu watoto kukoma kufanya hivyo akisema kuwa ni kinyume na mafundisho ya kanisa.

Akihubiri katika kanisa la holy Rosari Sing’ore katika maadhimisho ya siku maalum ya kuwasherehekea watoto waloiuawa na mfalme herode baada ya kristu kuzaliwa askofu Kimengich amewafananisha wale wanaowadhulumu watoto na Herode akitoa wito kwa kila mzazi na walezi wa watoto kuhakikisha kuwa watoto siku zote wanalindwa dhidi ya wale walio na hulka mbaya.

Askofu kadhalika aliwataka watoto kuishi maisha ya ukristu kwa kutii amri za Mungu akisema kuwa utiifu huo ndio ngao ya kuurithi ifalme wa mbinguni, huku akitoa wito kwa wazazi na wale wanaowalea watoto siku zote kuwaelekeza kwa Mungu kwa kupanda mbegu ya maadili maishani mwao.

Aliwataka watoto wa missionary jimboni kuanzisha zoezi la kuwatembelea watoto wanaougua katika hospitali na hata kuwa na hazina ya kuwasaidia wale wanaolemazwa na makali ya njaa katika sehemu mbalimbali kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *