Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameitaka serikali ya kitaifa kuweka mipango maalum za kuhakikisha maradhi ya Ebola haitashuhudiwa nchini.
Askofu Kimengich alisema kwamba serikali kupitia wizara ya afya kama hapo awali ilivyoweza kukabiliana na homa kali ya Corona inadhihirisha inaweza ikazuia Ebola kuingia nchini.
akiongea mjini Eldoret,Kimengich akiweka bayana kwamba mashirika mbalimbali ikishirikiana na sekta ya uchukuzi na la afya yajadili mbinu mwafaka za kuwaweka salama wakenya akieleza kwamba wakenya kwa sasa wanakabiliana na hali ngumu ya maisha na iwapo ugonjwa huo utaingia nchini itawahangaisha sana wakenya.
Aliwaomba wakenya nao kuzingatia matakwa yote yatakayotolewa na serikali hasa wale wanaoishi kwenye mipaka za Kenya na Uganda kukabili maradhi hayo.