CBC YASTAHILI KUFANIKISHWA

Wizara ya elimu imeshauriwa kuhangazia maswala tata kwenye sekta hiyo kukabiliana na changamoto ambazo huenda zikarudisha nyuma juhudi za kuimarisha sekta hiyo.


Akiongea mjini Eldoret,katibu wa muungano wa walimu tawi la Chepkoilel katika kaunti ya Uasin Gishu Sammy Bor amesema mfumo mpya wa elimu CBC imeingia wakati wizara haikua imeweka mikakati maalum na yastahili sekta kuwa mstari wa mbele kuweka hai matumaini ya kuendelea kwa mtaala huo.

Ameiomba serikali kupitia wizara ya Elimu kuwahusisha washikadau mbalimbali wanaohusika na elimu wakiwemo wazazi,walimu,wanafunzi na washikadau wengine ndipo waweze kuafikia mfumo huo kikamilifu.

Aidha,katibu huyo aliitaka wizara hiyo ya elimu kuwapa mafunzo ya kutosha kwa walimu kuhusu CBC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *