PADRE OPONDO :masomo kwa wanafunzi wote

Wito umetolewa kwa walimu na wasimamizi wa shule kubuni mbinu mbadala za kuhakikisha wanafunzi wanasalia shuleni licha ya hali ngumu ya uchumi.

Akizungumza afisini mwake mjini Eldoret, katibu wa elimu katika jimbo katoliki la Eldoret Padri Rafael Opondo aliwapongeza wanafunzi waliorudi shuleni licha ya changamoto za karo kutokana na hali ngumu ya maisha.

Aliwarai walimu na wasimamizi wa shule kushauriana na wazazi kuhusu namna watakavyolipa karo pasi na kutatiza masomo ya wanafunzi.

Wakati uo huo, Padri Opondo akisisitiza umuhimu wa walimu, wazazi na wanafunzi kushirikiana kwa karibu ili kuweka mazingira bora kwa watahiniwa kujiandaa mitihani ya kitaifa.

Aidha, aliwashauri wanafunzi kuwa na nidhamu kuweka fikira zao zote kwenye masomo licha ya hali ngumu ya maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *