BISHOP MAKUMBA; Uaviaji Mimba ni Dhambi

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba alitoa wito kwa waumini  kujiepusha na matendo maovu ambayo yanaathiri kizazi cha sasa na kijacho.

Akihuburi katika misa ya siku ya maombi ya kitaifa katika eneo la Subukia jimbo katoliki la Nakuru, askofu mkuu Muhatia alishtumu vikali mashirika ambayo yamekuwa yakishinikiza miswada na sheria ambazo zinashabikia uaviaji wa mimba na ndoa ya jinsia moja, akitoa wito kwao kujiepusha na miswada hizo, kwa kuwa zinaathiri kizazi kijacho na kwenda kinyume na mafunzo ya kanisa.

Askofu Muhatia alitoa wito kwa waumini kwa jumla kuwa watiifu kwa kumfuasa Yesu, kwa kuwa huyo kristu ndio anayesamehe dhambi na kupyaisha binadamu wakati ambapo ameteleza kwa kutenda yasiyompendeza mwenyezi Mungu.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni binadamu wanaotembea pamoja kwa kutunza mazingira akiwataka kila mkenya na kila mkristu kutunza mazingira na kutumia akili aliyojaliwa na Mungu  kwa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *