BISHOP KIVUVA : Taifa lisonge mbele

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB limetoa wito kwa wakenya kuweka kando tofauti zao  waliokuwa nao wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, na badala yake kukumbatiana na kuendelelea kushirikiana kwa pamoja kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa askofu Martin Kivuva Musonde, aliwashukuru wakenya kwa kushiriki zoezi la kupiga kura na kuyapokea matokeo hayo kwa amani, na kutoa wito kwa viongozi kuwa waadilifu kwa kuwatekelezea wakenya yale waliyoahaidi wakati wa kampeni .

Baraza hilo likitoa wito kwa viongozi wote waliochaguliwa na wale hawakuchaguliwa kukumbatiana na kushirikiana kwa kuanagamiza jinamizi la ufisadi ambayo kwa sasa limeshika mateka taifa hili.

Mwezi huu wa kumi ikiwa ni mwezi wa mama Maria askofu Kivuva alitoa wito kwa wakenya kuendelea kuhiji meaner ya kuabudu kwa kusali kwa ajili ya familia na wakenya kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *