Oparesheni ya kwa jina ‘Komesha Uhalifu’ inayofanywa na asasi za kiusalama katika eneo la North Rift imepiga hatua kubwa katika kaunti za Baringo na Turkana.
Huduma ya polisi ka taifa kupitia mtandao wao wa twiiter imesema tayari imefaulu kupata bunduki na risasi kadhaa.
Oparesheni hiyo ilianzishwa kufuatia shambulizi katika kaunti ndogo ya Turkana Mashariki ambapo watu 11 walipoteza maisha yao.
Maafisa wa usalama wanane, raia wawili na chifu mmoja ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulizi halo ambalo lilikashifiwa kote nchini.
Huduma hiyo imesema imeongeza idadi ya maafisa wa polisi ambao watahakikisha silaha zilizoibwa zimesalimishwa na kuhakikisha utulivu umerejea.
Aidha Huduma hiyo ilipongeza wananchi kwa kuwaunga mkono na kuwata kutoa ripoti zitakazochagia kufanikisha operasheni hiyo.