Gavana wa kaunti ya Siaya James Orengo amemuagiza katibu wa kaunti hiyo Joseph Ogutu na maafisa wote wakuu wa kaunti hiyo kwenda likizo ya lazima.
Hatua hiyo inakusudiwa kulipa jopo kazi la kuchunguza shughuli za kifedha za serikali ya kaunti hiyo muda wa kutosha wa kukamilisha kazi yake.
Gavana huyo pia amefanya mabadiliko katika idara ya fedha ya kaunti hiyo na akamteua Richard Mungla kuwa afisa mkuu mpya wa kifedha.
Orengo pia aliwahimiza watu wa kaunty ya Siaya kulipa jopokazi hilo raslimali linalohitaji ili liweze kutekeleza kazi yake ipasavyo.
Ameitaka tume ya kukabiliana na ufisadi humu nchini na idara ya upelelezi ambazo kwa wakati huu zinachunguza matumizi mabaya ya pesa za kaunti hiyo zikamilishe haraka uchunguzi wao ili waliohusika wachukuliwe hatua.
