Muungano wa wafanyibiashara knicc tawi la Uasin Gishu umeitaka bunge la kaunti hiyo kuharakisha kupitisha sheria itakayotoa mwongozo wa namna sekta ya kibinafasi itaweza kushirikiana na serikali ya kaunti hiyo ili kuimarisha uwekezaji.
kulingana na mwenyekiti wa muungano huo Willy Kenei akiongea wakati wa mkutano na uongozi wa kaunti ya Uasin Gishu ukiongozwa na gavana Jonathan Bii na wafanyibiashara ambako waliitaka kuboreshwa mazingira ya kibiashara mjini eldoret, huku wakiahidi kushirikiana na kaunti kuhakikisha mji wa Eldoret unapandishwa ngazi na kuwa jiji chini ya mwaka mmoja ujao.
Gavana Chelilim kwa upande wake aliahidi kuboresha hali ya usalama mjini humo na pia kuboresha mazingira ya viwanda na biashara na hata utalii .