SHEREHE YA WANAFAMASIA

Wito umetolewa Kwa wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu kutafuta ushauri kutoka Kwa wataalam wa afya Kwa matumizi ya dawa iwapo hawajazuru hospitalini Kwa matibabu.


Wakiongea mjini Eldoret,wahudumu wa afya hasa wanaphamasia waLIwahimiza wenyeji kutonunua tu madawa ovyo bila ya kupewa maelekezo Kwa wanachosema huenda ikaathiri afya Yao Kwa hili akiwaomba kuwa waangalifu.


Wakiongozwa na Dkt.Barbara Chepkorir msimamizi wa wanaphamasia kwenye hospitali ya District kaunti ya Uasin Gishu na Dkt.Henry Amdany waliwakumbusha wakaazi kwamba utumizi wa madawa bila maelekezo ni hatari mno kwa usalama Afya Yao.

Walisema wataendelea kuhimiza na Kuwahamashisha wenyeji jinsi ya kudhibiti magonjwa Sugu ikiwemo kisukari na magonjwa mengine yanayohitaji mgonjwa kutafuta dawa Kila mara bila kuzuru hospitali.

Ikumbukwe wanaphamasia hao walizungumzwa wakati ulimwengu ukisheherekea siku ya phamasia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *