CHELILIM:elimu bora kwa wasiokuwa na makao

Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imesema imeweka mikakati za kutosha kuhakikisha watoto wasiokuwa na makao hasa wanaoishi kwenye makao ya uokozi wanapata Elimu Bora.


Akiongea wakati alipozuru eneo hilo viungani mwa mji wa Eldoret Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Chelilim Bii alisema watoto hao wanahitaji la kupata Elimu ,makaazi ,chakula na hata mavazi na kama Serikali watafanya Kila wawezalo kuwahakikishia hali Bora ya maisha hapo baadae.

Aliwataka wahisani kujitokeza kuunga mkono juhudi za Kaunti kuwapa makao watoto wasio na makwao.


Wakati huo aliwaomba familia ambazo wanao walitorokea mitaani kuwarudisha wanao makwao kurahisishia Serikali kazi yake ya kuwahifadhi wasiokuwa na makao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *